fbpx CARNEGIE AFRICAN DIASPORA FELLOWSHIP PROGRAM (CADFP) Yateua Kuufadhili Mradi wa UoK | University of Kabianga | Innovation and Excellence

University of Kabianga (UoK) imet̪unukiwa ufadhili wa mrad̪i wake wa kimasomo kut̪oka Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP) katika duru ya ufadhili wa Shit̪aa 2022.

Tangazo rasmi la ut̪euzi huu, mnamo Aprili 2022, limearifu kuwa walimu Prof. Jonathan Choti wa Michigan State University (MSU), kutoka Marekani, na Dkt. Mohamed Karama wa UoK, Kenya, wamebahat̪ikiwa kut̪euliwa katika duru ya ufadhili mwaka huu. Mrad̪i wa UoK ulifaulu kuwashawishi CADFP kuukubali na kuufadhili juu ya maombi mengi yaliyotumwa kutoka Afrika nzima na ufadhili kupunguwa.

Mrad̪i wenyewe wahusu ushirikiyano baina ya Prof. Choti na walimu wa Kit̪engo cha Kiswahili UoK katika kuunda pamoja kozi za Kiswahili kama Lugha ya Kigeni, shughuli inayofanyika kwa mara ya kwanza katika vyuwo vya humu nchini Kenya. Piya, wahusu kutiliya nguvu na kukarabat̪i mit̪aala ya masomo Kiswahili ya UoK katika d̪araja ya Digrii ya Awali na Baad̪a ya Ijaza. Zaid̪i ya hayo, Walimu na wanafunzi wa ngazi za Uzamili na Uzamifu wat̪anufaika kwa warsha na mafunzo yat̪akayot̪olewa na mt̪aalamu Choti katika mawanda ya Isimu na Ut̪afit̪i wake.

Ut̪akapokamilika, mrad̪i huu unat̪arajiwa kufaid̪i walimu, wanafunzi na vyuwo vyot̪ʰe viwili (UoK & MSU) katika ushirikiyano wa kimasomo, kiut̪afit̪i katika Kiswahili bali katika mawand̪a yot̪ʰe yanayoleta faid̪a kwa ummah. T̪ayari kuna mazungumzo ya ushirikiyano baina ya vyuwo hivi viwili kuhusu ubad̪ilishanaji wa wanafunzi na walimu, ushirikiyano kuwaleta wanafunzi wa MSU kuja kusoma Kiswahili na Ut̪amad̪uni wake huku UoK, na matarajiyo ya ushirikiyano kukuwa kufikiya mawanda yot̪ʰe ya kiushirikiyano. Isit̪oshe, UoK inajiweka t̪ayari katika kujitangaza kuwa mahala pa masomo ya Kiswahili kama Lugha ya Kigeni kwa ulimwengu mzima ikizingat̪iwa kuwa Kiswahili ni Lugha ya Ulimwengu sasa.

Mrad̪i wa ushirika wa CADFP huwat̪euwa wasomi wanaosomesha ughaibuni kuja kuwapa wenziwao wa Afrika ut̪aalamu waliyoukusanya huko ughaibuni kufaidi Afrika na nchi zao za uzawa. Wat̪aalamu hawa huwa wamebobeya katika mawand̪a yao na hut̪euliwa kama njiya moja ya kurejesha fadhila za asili ya usomi wao. Kila mwaka kuna duru za ufadhili na kila chuwo katika Afrika huombwa kutuma ombi la ufadhili wa mrad̪i wake ili kunufaisha chuwo hicho na nchi kwa jumla. Mara hii ni zamu ya UoK na MSU!

English Translation

The University of Kabianga (UoK) has been awarded a sponsorship for its project from the Carnegie African Diaspora Fellowship Program (CADFP) in the Winter 2022 funding cycle.

Announced in April 2022, Prof. Jonathan Choti of Michigan State University (MSU), United States, and Dr. Mohamed Karama of UoK, Kenya, were one of the lucky nominees for the sponsorship this year despite increased number of applications from across Africa and reduced donor funding.

The project is a collaboration between Prof. Choti and faculty members of the UoK Kiswahili Unit in co-developing Kiswahili as a Foreign Language courses, a first in universities here in Kenya. Also, strengthening and revamping the UoK Kiswahili curriculum in the Undergraduate and Postgraduate degrees. In addition, UoK Kiswahili lecturers and postgraduate students will benefit from the workshops and training provided by Choti in his field of Bantu linguistics and research.

This project is expected to benefit both lecturers, students and the universities (UoK & MSU) in academic, research cooperation in Kiswahili and in all fields that benefits humanity. Talks between the two institutions on student & faculty exchanges, a partnership to bring MSU students to study Kiswahili and its culture at UoK, and other partnerships in all areas of cooperation have begun and are expected to be completed with a MoU. In addition, UoK is positioning itself as a suitable destination of learning Kiswahili as a Foreign Language for the whole world considering that Kiswahili is now a World Language.

Every year CADFP selects diaspora scholars to give their African counterparts the expertise they have accumulated abroad to benefit Africa and their native countries. These professionals are experts in their fields and are nominated by an Advisory Council. Every year there are calls for funding by CADFP and institutions in Africa are invited to submit project request(s) to benefit them and the country as a whole. Bravo UoK and MSU!

Translation

 

Connect with us